Ijumaa , 21st Oct , 2022

Mkuu wa wilaya ya Nzega, mkoani Tabora Kamishina Msaidizi wa Polisi Advera Bulimba, amesema hayuko tayari kuona unafanyika ubadhirifu wa fedha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mkuu wa wilaya ya Nzega, Kamishina Msaidizi wa Polisi Advera Bulimba

Akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji na miradi  pamoja na mapokezi ya fedha  kwa  wilaya  hiyo tangu kuingia madarakani kwa Rais Samia Suluhu Hassan, amesema  zaidi ya shilingi billion 97 zimepokelewa katika wilaya ya Nzega kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Amesema mpaka sasa wilaya ya Nzega inaendelea na utekelezaji wa miradi ya kimkakati kupitia fedha hiyo katika sekta ya elimu, afya, maji na umeme lengo ikiwa ni kuendelea kuboresha na kusogeza huduma kwa wananchi wa wilaya ya Nzega.