Jumanne , 25th Oct , 2022

Uongozi wa klabu ya Yanga umekanusha vikali taarifa za kumfuta kazi Kocha wake Mkuu Mtunisia Mohamed Nasreddine Nabi baada ya tetesi kuzagaa kuwa Kocha huyo ameshatimuliwa kazi ndani miamba hiyo ya Jangwani

Mtendaji Mkuu wa Yanga, Mzambia  Andre Mtine amekanusha taarifa hizo za kuachana na kocha Nabi na kusema bado wanaendelea na mkufunzi huyo ambaye ameiongoza Yanga kutwaa mataji 3 mpaka sasa huku akijivunia rekodi ya kutofungwa kwenye michezo 43 ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara

“Niwaombe mashabiki na wanachama wetu kuwa na utaratibu wa kufatilia taarifa za klabu yetu kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari,tuna kurasa zetu za mitandao ya kijamii ambazo zimekuwa zikitoa taarifa za klabu yetu na kwa wakati sahihi,” amesema Mtine

Yanga inataraji kushuka dimbani kesho Jumatano Oktoba 25-2022dhidi ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 19:00 Usiku