Ijumaa , 28th Oct , 2022

Mwanamke aliyemuua na kumkatakata tamaa rafiki yake kabla ya kumuweka kwenye sanduku na kuutupa mwili amehukumiwa kifungo cha maisha jela.

 

Jemma Mitchell atatumikia kifungo cha maisha jela  kwa kumuua Mee Kuen Chong mwenye umri wa miaka 67 nyumbani kwake London mnamo Juni 2021.

Jaji aliyetoa hukumu hiyo Richard Marks ,siku ya leo amesema kwamba  Bi Chong, jaji alisema aliuawa kikatili sana, na amemwita mwanamke huyo kuwa muovu.

  Mitchell anakuwa muuaji wa kwanza na mwanamke wa kwanza kuhukumiwa kwenye televisheni nchini Uingereza na Wales, hiyo ni baada ya sheria kubadilishwa ili kuruhusu kamera kuingia katika vyumba vya mahakama.

Mwili wa Bi Chong ulipatikana katika maeneo ya misitu huko Salcombe na mpita njia,  na kichwa chake kiligunduliwa karibu siku chache baadaye. 

Mwanapatholojia aliyefanya uchunguzi wa maiti dhidi ya Bi Chong hakuweza kubaini chanzo cha kifo kwa sababu ya kiwango cha kuharibika, lakini aliweza kubaini kuvunjika kwa fuvu lake.