
Miili ya watumishi wa MDH waliofariki kwenye ajali ya ndege Bukoba
Rashid Mfaume Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akimwakilisha Waziri wa Afya anabainisha kuwa watumishi hawa wamekuwa na mchango mkubwa katika kukabiliana na kudhibiti magonjwa ya mlipuko nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa MDH akaeleza namna watumishi hao walivyoacha pengo kubwa, kutoka na mchango wao mkubwa katika kuhakikisha watu wanakuwa na afya nzuri.
Watumishi walioagwa leo jijini Dar es salaam, walifariki asubuhi ya Novemba 6,2022 katika ajali ya ndege ya shirika la ndege la precision Bukoba Mkoani Kagera.