Jumatatu , 21st Nov , 2022

Chama cha Mapinduzi CCM kimefuta uchaguzi wa umoja wa vijana mkoa wa Simiyu kutokana na tuhuma za rushwa zilizoibuliwa

Katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo amesema pia chama hicho kimesimamisha uchaguzi wa nafasi ya mjumbe wa hammashauri kuu mkoa wa Mbeya, na Arusha pamoja na uchaguzi uliofanyika jana mkoa wa Magharibi Zanzibar 

Amesema hatua hiyo inapisha uchunguzi ambao tayari umeanza juu ya tuhuma mbalimbali zilizoibuliwa ikiwemo rushwa