
Mashahidi hao ni Neema Julian ambaye ni mshitakiwa namba 5, Geoge Maloji ambaye ni mshitakiwa namba 8, pamoja na Isaka Mashaka mshitakiwa namba 4 katika kesi hiyo.
Akitoa ushahidi wake Neema Julian ameieleza mahakama kuwa yeye hujishughulisha na usafi nyumbani kwa Mfalme Zumaridi na kwamba siku ya Februari 23/2022 hakujua kilichotokea kwani alikuwa akimwagilia maua nje ndipo akaona gari la polisi likiingia nyumbani kwa Zumaridi na kuwakamata
Aidha ameieleza mahakama kuwa maelezo yaliyowahi kutolewa makamani kama ushahidi si yake kwani aliyakuta mahakamani hivyo anachokumbuka akiwa polisi aliulizwa majina yake, umri, kazi yake na mahala anapoishi.
Shahidi mwingine George Maloji ameieleza mahakama hiyo kuwa alikamatwa Februari 26 mwaka huu akiwa nyumbani kwa Zumaridi akiuza nguo kwani yeye ni machinga hivyo alifika hapo siku hiyo kwa lengo la kutafuta wateja wa biashara yake.
Ameongeza kuwa anakumbuka siku ambayo Inspekta Zongo alitoa ushahidi wake alidai mahakamani hapo kuwa anamtabua kwa kuwa alimwandika maelezo lakini alishangazwa na kitendo cha kuionyesha mahakama maelezo yasiyo na jina lake baali yana jina lingine.
Naye Isaka Mashaka fundi ujenzi akitoa ushaidi wake ameieleza mahakama kuwa kabla ya kukamatwa Februari 26 ,2022 alisikia kishindo cha geti kuvunjwa pamoja na milio ya risasi ndipo akakamatwa na Askari polisi na kuacha kazi yake ya ujenzi iliyompeleka nyumbani kwa mhubiri huyo.