
Hatua hiyo itasaidia kutatua kero na kilio cha wananchi wa vijiji 18 vilivyopo mwambao wa Ziwa Nyasa ambavyo havijawahi kupata ya maji ya bomba safi na salama tangu vianzishwe
Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa Mhandis Kivegalo akiwa ziarani wilayani Ludewa kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita baada ya kutolewa fedha kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 7.4 kwenda kutatua changamoto ya ukosefu wa maji kwa wananchi wilayani humo, ambapo Meneja wa Ruwasa wilaya ya Ludewa, Mhandisi Mlenge Katulilo akisoma taarifa mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa amekiri kuwa vijiji 17 vilivyopo mwambao wa ziwa Nyasa havijawi kupata maji safi na salama
Kufuatia hali hilo ndipo Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa Mhandisi Kivegalo ame maelekezo kwa Meneja wa Ruwasa wilaya ya Ludewa akiwa katika eneo la mradi wa ujenzi wa matenki ya maji yaliyopo Kata ya Ludewa mjini yaliyofikia asilimia 15 hadi sasa ili kutatua kero ya uhaba wa maji mjini Ludewa.
Imeelezwa kukamilika kwa ujenzi wa matenki makubwa mawili ya mradi wa usambazaji maji katika kata ya Ludewa mjini unatarajiwa kuwahudumia wananchi elfu 15660 hali ambayo baadhi ya wananchi wameishukuru serikali.