Jumatano , 30th Nov , 2022

Asilimia 95 ya wakimbizi na waomba hifadhi wa nchi ya  Burundi wanohifadhiwa katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu Kasulu mkoani Kigoma, wamegoma kurejea nchini mwao kwa kile wanachodai bado hali ya amani hairidhishi na kuomba serikali ya Burundi kuwahakikishia amani ili waungane na wenzao.

Wakimbizi

Mkuu wa kambi ya wakimbizi Nyarugusu Siasa Manjenje, amesema hayo wakati wa mkutano wa viongozi wa idara ya wakimbizi kutoka Tanzania na Burundi na kamati za ulinzi na usalama kutembelea kambini hapo, huku wakimbizi wenyewe wakieleza sababu kuwa, hawaamini hali ya usalama kuimalika nchini mwao.

Kwa upande wake Mkurugenzi idara ya huduma kwa wakimbizi nchini, Sudi Mwakibasi, amewataka wakimbizi kuendelea kurejea kwa kasi na kulingana na Warundi wenzao katika Kujenga Taifa hilo.

Aidha Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye, na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Burundi Nibona Bonansize , amewahakikishia wakimbizo hao nchi ya Burundi kuwa shwari na kwamba hawana budi kuendelea kuishi kama wakimbizi mbali wakajenge nchi yao.