
Maandamano hayo makubwa katika mji mkuu yaliandaliwa na chama cha upinzani cha Bangladesh Nationalist Party (BNP), ambacho kinamshutumu Hasina kwa kushindwa kushughulikia kupanda kwa bei ya mafuta na gharama ya maisha.
Maandamano ya Jumamosi yanakuja wakati kukiwa na maandamano mengi nchini Bangladesh ya kumtaka Hasina kujiuzulu na kudai uchaguzi mpya..
Hasina amejibu kwa kuwaita viongozi wa upinzani "magaidi" na kuwaonya watu dhidi ya kuruhusu BNP - chama kikubwa cha upinzani - kurudi madarakani.Watu kadhaa walikamatwa kuelekea maandamano ya Jumamosi.
Polisi waliwakamata viongozi wawili wakuu wa BNP, akiwemo katibu mkuu wa chama hicho Mirza Alamgir siku ya Ijumaa. Maafisa walisema Alamgir alikuwa akikabiliwa na mashtaka, bila kutoa taarifa zaidi.