
Timu zingine zilizopangwa kwenye kundi hilo ni US Monastir ya Tunisia na Real Bamako ya Mali.
Hatua ya makundi ya michuano hiyo ya kombe la Shirikisho Afrika inatarajiwa kuanza Februari 12 mwakani hivyo wanamiezi miwili ya kujiandaa na patashika hizo.
Mara ya mwisho kwa Yanga kushiriki kombe la Shirikisho ilikuwa 2018 ambapo ilitinga hatua ya makundi lakini waliishia kuburuza mkia kwenye kundi D wakiwa na pointi nne nyuma ya Gor Mahia ya Kenya, Rayon Sports ya Rwanda na USM Alger ya Algeria.
Wananchi watapata nafasi ya kuliona chama lao likicheza hatua hiyo baada ya miaka mitano kupita huku wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri kutokana na ubora wa kikosi chao ambacho kimetinga hatua hiyo baada ya kuing'oa Club Africain ya Tunisia.