Alhamisi , 16th Feb , 2023

Uongozi wa klabu ya Azam Fc umesema bado upo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wa 2022-23 licha ya kuzidiwa alama 16 na kinara wa ligi hiyo klabu ya Young Africans.

Azam Fc

Akizungumza na EATV, Afisa Habari wa Azam FC Hasheem Ibwe amesema bado wapo kwenye harakati za kuhakikisha wanaondoka na alama 3 kwenye michezo 8 iliyosalia huku akisifu uwezo wa kikosi chao

''Tuna kikosi imara naamini tutapata matokeo mazuri ambayo yatatuweka katika nafasi nzuri ''Hasheem Ibwe 

Kwa upande mwingine ,Ibwe ameelezea maandalizi ya kikosi chao kuelekea michezo iliyosalia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo imesimama kidogo kupisha ushiriki wa klabu za Simba na Yanga kwenye michuano ya kimataifa

Azam Fc inakamata nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara wakiwa na alama 43 huku mchezo unaofuata kwenye mzunguko wa 24 watapambana na Simba SC mnamo Februari 21-2023 kwenye dimba la Benjamin Mkapa majira ya Saa 19:00 Usiku