Sekiete Selemani, aliyetumbuliwa
Sekiete ametenguliwa kwenye nafasi hiyo tangu Aprili 16, 2023.
Januari 27 mwaka huu, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima, alipokea ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za kuuza viwanja vya serikali vilivyokuwa vikidaiwa kuuzwa kwa shilingi bilioni 1 kinyume na taratibu na Mkurugenzi wa jiji hilo Selemani Sekiete, viwanja vilivyopo Halmashauri ya wilaya ya Nyamagana mkoani humo.
Viwanja hivyo viwili vya serikali namba 194 na 195 vinavyodaiwa kuuzwa kwa shilingi bilioni 1, vilipelekea mkuu wa mkoa huo wa Mwanza Adam Malima, kumshtaki Mkurugenzi huyo Ofisi ya Rais TAMISEMI na kwamba watumishi wanne walisimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa uuzwaji wa viwanja hivyo.

