
Pesa hiyo ni bonus kwa mujibu wa mkataba ambapo wakifanikiwa kuingia hatua hiyo M-bet kama wadhamini wakuu wanapaswa kutoa kitita hicho.
Meneja Masoko wa M-bet, Alan Mushi amesema wanajivunia kufanya kazi nasi na uwepo wao kwetu unaendelea kutufanya kuwa imara zaidi na kupata mafanikio makubwa.
“M-bet inakabidhi hundi ya Sh. 100,000,000 kwa Simba kwa kufanikiwa kuingia Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni bonus kwa mujibu wa mkataba. M-bet tunajivunia kufanya kazi na Simba na tunaamini uwepo wetu utawafanya kupata mafanikio zaidi,” amesema Mushi.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amewashukuru M-bet kwa kutimiza makubaliano kwa mujibu wa mkataba.
“Mpira wa miguu unahitaji uwekezaji mkubwa na M-bet mmefanya jambo zuri kiasi hiki kimetuongezea hamasa,” amesema Kajula.