
Mwamuzi wa Ujerumani Felix Zwayer
Zwayer mwenye umri wa miaka 43 alifungiwa kwa miezi sita mwaka 2006 baada ya kuchunguzwa kwa kupokea hongo ya pauni 250 ambayo ni sawa 745,950 kwa fedha ya Tanzania liyopokea kutoka kwa mwamuzi mwenzake Robert Hoyzer ambaye baadaye alifungiwa maisha.
Zwayer ambaye amekana kufanya makosa hayo alikuwa mmoja wa maafisa walioarifu mamlaka ya soka juu ya mpango wa upangaji matokeo wa Hoyzer na kupunguziwa adhabu kwa kufungiwa kwa muda mfupi.
Baada ya kufungiwa Zwayer amekuwa mmoja wa waamuzi wazuri barani Ulaya na ndiye aliyechezesha mechi ya Arsenal katika mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Paris St-Germain Jumatano iliyopita.