Jumatano , 22nd Oct , 2025

"Kauli ya Rais Samia imekuja kuzima hofu iliyotanda na kuwataka Watanzania kutumia siku hiyo kutimiza uhuru wao wa kuchagua Viongozi wanao wataka badala ya kusikiliza maneno ya watu ambao hawaitakii mema Tanzania."

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama Cha UNITED PEOPLE'S DEMOCRATIC PARTY Twalib Kadege amewasihi Watanzania kujitokeza Kwa Wingi tarehe 29 kwenda kupiga kura huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwatoa hofu Watanzania kupiga kura kwa amani Oktoba 29 mwwaka huu.

Kadege ameyasema hayo akirejelea kauli ya juzi Oktoba 20 ya Dkt. Samia katika mkutano wa kampeni aliofanya Jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kauli ya Rais Samia imekuja kuzima hofu iliyotanda na kuwataka Watanzania kutumia siku hiyo kutimiza uhuru wao wa kuchagua Viongozi wanao wataka badala ya kusikiliza maneno ya watu ambao hawaitakii mema Tanzania.

Mgombea huyo wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia UPDP ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa Jimbo la Bagamoyo katika uwanja wa Top Top.