Uchunguzi wabaini The Cask ilichomwa na watu
Siku tatu baada ya baa maarufu ya The Cask iliyopo ndani ya jengo la kibiashara la Rock City Mall kuteketea kwa moto, Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mwanza limebaini chanzo cha kuzuka kwa moto huo kuwa ni hujuma iliyofanywa na watu wasiojulikana bila kuwepo kwa sababu yoyote.