''Tanzania imepiga hatua kidijitali'' - Munaku
Mkurugenzi wa Tehama na Mwenyekiti wa Kongamano la Tano la Mkutano Mkuu wa Tehama 2021, Mulembwa Munaku, amesema Tanzania kwasasa imepiga hatua kama taifa kwenye matumizi ya Tehama na jitihada zinaendelea kuhakikisha hatua nzuri zaidi inafikiwa.