Wazee wasiojiweza watapatiwa huduma zote- Serikali
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, anayeshughulikia Maendeleo ya Jamaii Dkt. John Jingu amesema Wizara hiyo itahakikisha inatekeleza kikamilifu agizo la Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan la huduma kwa makundi maalum ya watoto na Wazee wasiojiweza.