Thaddeo Lwanga kuikosa Dodoma Jiji
Klabu ya soka ya Simba itamkosa kiungo wake mahiri Thaddeo Lwanga kwenye mechi ya kesho Ligi Kuu ya Tanzania bara dhidi ya Dodoma Jiji kutokana na kuendelea kuwa nchini mwao Uganda baada ya kufiwa na dada yake wiki iliyopita.