Tusione kifungashio kisichokuwa na viwango - NEMC
Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC) limesema kuwa kuanzia kesho Jumatatu ya April 19 vifungashio visivyokuwa na ubora ambavyo vimezuiwa kutumika havitakiwi kuonekana sokoni na endapo Mfanyabishara au mteja akimatwa adhabu yake ni faini au kifungo jela.