"Hakuna jambo litakaloharibika"- Rais Mh. Samia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu, amewaomba Watanzania kushikamana katika kipindi hiki na kwamba wasiwe na hofu kwani Tanzania inayo hazina nzuri ya viongozi wakiwemo waliostaafu hivyo hakuna jambo litakaloharibika.