Real, City ndiyo kusema nusu fainali inawahusu?
Klabu za Real Madrid na Manchester City jana zilipata ushindi katika michezo yake ya mkondo wa kwanza wa ligi ya mabingwa Ulaya iliyopo katika hatua ya robo finali, hivyo kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya nusu fainali.