Hatimaye Yanga yakubali kipigo cha kwanza VPL.
Vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga, jioni ya leo tarehe 5 Machi 2021, imepoteza mchezo wake wa kwanza msimu huu kwenye ligi hiyo baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wa mchezo huo, klabu ya Coastal Unioni kwenye dimba la Mkwakwani jijini Tanga.