ACT wataja sababu za kumchagua Othman Masoud
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amesema kuwa waliamua kumpendekeza Othman Masoud, awe mrithi wa Maalim Seif, kwa sababu ya misimamo yake na uwezo wake uliojipambanua kuhusu maslahi ya Zanzibar na ni mtu ambaye hakutaka sifa za kisiasa.