Samaki waliokufa waibua hofu Ziwa Victoria
Wakazi wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, wamekumbwa na hofu ya kulishwa samaki wanaookotwa ziwani na wavuvi wakiwa wamekufa, baada ya kuonekana uwepo wa samaki wengi wanaoelea katika ziwa Victoria, ambao chanzo cha kifo chao bado hakijafahamika.