Moto wateketeza mabweni shule ya Sangiti
Wanafunzi 180 katika shule ya sekondari ya wasichana Sangiti iliopo kata ya Kirima Kibosho wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamenusurika kifo baada ya mabweni manne ya kidato cha tatu na cha nne ya shule hiyo kuteketea kwa moto na kuteketeza samani pamoja na mali za wanafunzi.