Magufuli awapa siku 7 Waziri Gwajima na Jafo
Rais Dkt John Magufuli, amewapa siku 7 Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, kuhakikisha wanaweka usawa katika suala la ugawaji wa madawa kwa mkoa wa Geita, kwani licha ya kwamba bajeti ya dawa imeongezeka lakini mkoa huo umekuwa ukipata dawa chache.