Serikali yatoa neno kuhusu zuio la Uingereza
Mkurugenzi wa Habari Wizara ya Mambo ya Nje, Emmanuel Buhohela, amesema kuwa wao hawana taarifa rasmi kwamba Uingereza imepiga marufuku wasafiri kutoka nchini Tanzania kuingia nchini humo na kueleza kuwa hayo ni mambo ya mitandaoni na wao hawayafuatilii.