Mkurugenzi aelekeza wenyeviti 8 kukamatwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu, Fabian Manoza, ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani wenyeviti wa vitongoji 8, katika Kata ya Itinje wilayani humo, wanaodaiwa kula fedha za michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari ya Kata hiyo.