Askari aliyeokoa mtoto hakuwa eneo lake la kazi
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Koplo Denis Minja, ambaye mwezi Mei alimwokoa mtoto mchanga akiwa hai ndani ya shimo la choo wilayani Ngara mkoani Kagera, amemwokoa tena mtoto mwingine wa kiume mwenye umri wa miaka 2, kutoka katika shimo la choo, eneo la Kayanga wilayani Karagwe.