Askari avumilia kipigo kwa miaka 4, RPC azungumza
Askari wa Jeshi la polisi mkoani Mwanza, Juliana Kwayi, ameamua kuvunja ukimya na kuviomba vyombo vya dola kumchukulia hatua za kisheria mume wake anayefahamika kwa jina la Nicolus Laurent, kufuatia mwanaume huyo kuwa na tabia ya kumpiga mara kwa mara na kumsababishia majeraha.