GEITA: Wanafunzi watumia mitumbwi kwenda shuleni
Wanafunzi wa Kisiwa cha Izumacheki kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Geita, mkoani Geita, wanalazimika kuvuka maji kwa kutumia mitumbwi inayosafiri kwa muda wa nusu saa kwenda shuleni, Kata ya Nkome, kutokana na eneo wanaloishi kutokuwa na shule, kitendo kinachohatarisha usalama wao.