Taarifa mbaya kuhusu Mbwana Samatta
Nahodha na mshambuliaji tegemeo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta atakosekana katika mechi ijayo dhidi ya Tunisia ambayo ni ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwakani kufuatia kupata majeraha ya nyama za paja.