Mawaziri wa fedha wa G7 wakutana kuijadili Ukraine
Mawaziri wa fedha wa nchi zilizostawi kiviwanda duniani za G7 wanakutana nchini Canada kwa mazungumzo yanayojikita katika mzozo wa Ukraine na kuyumba kwa uchumi wa dunia kulikosababishwa na ushuru uliowekwa na rais wa Marekani Donald Trump.