CHADEMA yatoa wito kwa vijana nchi nzima
Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) limewataarifu vijana wote wa chama hicho kuwa tayari muda wowote kutekeleza maagizo ya viongozi wao huku wakililalamikia Jeshi la Polisi kwa kutomwachia kiongozi wa baraza hilo, Patrick Ole Sosopi pamoja na Daniel Naftal.