Kiongozi wa Serikali auawa, DC afunguka
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ibambilo Kata ya Bulega Wilayani Bukombe Mkoani Geita,Juma Maziku, amefariki dunia saa chache baada ya kuokotwa akiwa ametupwa kwenye barabara iendayo Mnekesi Wilayani Chato,huku mwili wake ukiwa na majeraha ya kushambiliwa na watu wasiojulikana.