Babu wa Loliondo aja na utabiri mpya
Takribani miaka 9 tangu kupungua kwa idadi ya watu waliokuwa wakifika katika kijiji cha Samunge, tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha kupata kikombe cha Babu, mchungaji aliyekuwa akitoa huduma hiyo Ambilikile Mwaisapile ameibuka tena na kutoa utabiri mpya.