Zitto ambana Waziri kuhusu 'usumbufu wa uraia'
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameitaka Serikali kuhakikisha inatoa kwa haraka vitambulisho vya taifa ili kuondokana na usumbufu wanaopata wananchi wanaoishi maeneo ya mpakani ambao wamekuwa wakisumbuliwa kuhusiana na suala la uraia.