Rais Magufuli atoa angalizo hili kwa viongozi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka viongozi wa kuteuliwa kuanzia ngazi ya ukuu wa mkoa mpaka ngazi za chini, kujenga ushirikiano na uhusiano mzuri baina yao ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao, vinginevyo hatasita kuchukua hatua.