Baadhi ya abiria wakilazmika kupanda magari ya mizigo maarufu kama Kirikuu baada ya mgomo wa madereva wa daladala Manispaa ya Bukoba.
Kamanda wa Polisi Bukoba, Revocatus Malimi amesema jeshi hilo linafuatilia mgomo wa madereva uliotokea kwenye manispaa hiyo kwa kile kilichodaiwa ni kupinga baadhi ya tozo zilizowekwa na manispaa hiyo.