Fahima (19) mbaroni kwa tuhuma za kutupa kichanga.
Tukio hilo linadaiwa kutokea tarehe 25 Desemba 2025 majira ya saa 11:00 alfajiri katika Mtaa wa Balyehela, ambapo mtuhumiwa anadaiwa kutupa kichanga hicho muda mfupi baada ya kujifungua juu ya paa la nyumba inayomilikiwa na Emmanuel Magina Murul, fundi wa kuchomelea vyuma.

