Mayanga atangaza kikosi Taifa Stars
Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania 'Taifa Stars', Salum Mayanga ametangaza majina ya wachezaji 22 watakaounda kikosi kinachokwenda kushindana kuwania Kombe la Cosafa nchini Afrika Kusini inayotarajiwa kuanza Juni 25 mwaka huu.