Ni ushindi wa Watanzania wote - Msuva
Baada ya timu ya Yanga jana kuifunga bao 5-1 timu ya Ngaya SC ya Comoro katika michuano ya klabu bingwa Afrika, mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva amefunguka na kusema kuwa ushindi wao huo umeiwakilisha Tanzania na siyo Yanga pekee.