Huu ndiyo ukatili kwa wanawake sehemu za kazi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amesema katika sehemu ya kazi, wanawake wamekuwa wakikabiliwa na vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa kiwango kikubwa.