Bunge kuanza na sakata la njaa na hali ya uchumi
Mkutano wa Sita wa Bunge unaanza Jumanne Januari 31, 2017 na kumalizika Februari 10, 2017 Mjini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano huo utaanza na kauli ya serikali kuhusu hali ya chakula pamoja na deni la taifa na hali ya uchumi nchini.