TANESCO watakiwa kuwafuata wateja nyumbani
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalimani, amelitaka shirika la Umeme nchini Tanzania(TANESCO), kuwafuata wateja baada ya wao kuwafuata ofisini ili nishati hiyo iwafikie watanzania wengi zaidi na kujikwamua kiuchumi.