MARA YAKANUSHA KUKAGUA WASICHANA WALIOKEKETWA.
Mkuu wa wilaya ya Butiama mkoani Mara Moses Kaegele amekanusha kauli inayotajwa kutolewa na mkuu wa mkoa huo kwamba wanafunzi wa kike watakaguliwa ili kubaini kama wamefanyiwa vitendo vya ukeketaji, kwenye mkutano uliohusisha wadau wa huduma na maendeleo ya jamii.