Tanzania yakopeshwa trilioni 1.8 na Benki ya Dunia
Benki ya Dunia imeiidhinishia Tanzania, mkopo wenye masharti nafuu pamoja na msaada vyote vikiwa na thamani ya dola za Marekani milioni 775, sawa na takribani shilingi za Tanzania trilioni 1.8 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa bajeti, kuboresha uchumi na huduma za afya.