Ccm kutekeleza ilani ya uchaguzi 2020
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuwatumikia wananchi na kwamba ilani ya uchaguzi ya 2020 inatekelezwa.

