"Toeni taarifa za kelele na mitetemo"- Waziri Jafo
Serikali imetoa siku saba kwa maeneo yote yanayofanya uchafuzi wa mazingira unaotokana na kelele na mitetemo kurekebisha changamoto hiyo na kulielekeza Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuyafungia maeneo yatakayokaidi maelekezo hayo.
